Rais Samia amtumia salamu za rambirambi Rais Dkt.Mwinyi kufuatia ajali ya boti

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi kufuatia vifo vya watu 10 waliofariki dunia katika ajali ya boti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Ni ajali iliyotokea Januari 4, 2022 katika eneo la Bahari ya Kisiwa Paza iliyopo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 5, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu.

"Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Richard Thadei Mchomvu, watu hao walikuwa wanatoka Chakechake kuelekea kwenye mazishi katika Kisiwa Paza Wilaya ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar.

"Mheshimiwa Rais Samia amemuomba, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa pamoja na marafiki na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Samia pia amewaombea kwa Mwenyenzi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news