NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MKUU wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka watumishi wa Serikali na viongozi kwa pamoja wasaidiane kupeleka taarifa sahihi kwa umma na watanzania kuhusu mambo yanayofanywa na Serikali ili kuepuka upotoshaji.
Mkuu wa Mkoa amesema hayo kwenye kikao kazi cha watumishi wa Halmashauri na Wilaya pamoja na taasisi kutoka Mkoa wa Songwe
"Kitendo cha kuwaachia viongozi tu ndio waweze kutoa ufafanuzi kwa mambo yote ambayo yamefanyika na Serikali tutakuwa hatujatimiza wajibu wetu vizuri kama viongozi na watumishi wa Mkoa wa Songwe,"amesema Mhe.Mgumba.
Mkuu wa Mkoa amesema inashangazwa unakuta mtumishi wa Serikali kwenye mitandao naye anaipinga mambo ya Serikali akiamini Serikali ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri au Mkuu wa Mkoa yeye anajiweka kando kwamba sio sehemu ya Serikali na badala yake anakuwa sehemu ya kuishambulia Serikali kwenye mitandao, "uko ni kutojutanbua kwa mtumishi wa Serikali".
Tags
Habari