Shule na wanafunzi waliovunja rekodi kumi bora Matokeo Kidato cha Nne 2021/2022,Kemebos yakomba 'division one' zote

NA GODFREY NNKO

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne uliofanyika mwaka 2021 huku asilimia 87.3 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wakifaulu. 
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde amewaeleza wanahabari leo Januari 15, 2022 jijini Dar es Salaam kuwa watahiniwa wa shule 422,388 sawa na 87.3 kati ya watahiniwa 483,820 wenye matokeo ya kidato cha nne wamefaulu mitihani yao muhimu kuingia katika elimu ya kidato cha tano. 

“Ufaulu wa watahiniwa umeongezeka kwa asilimia 1.46 ikilinganishwa na mwaka wa 2020,” amesema Dkt. Msonde.

Aidha, Dkt. Msonde amesema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa umechunguzwa na kubainishwa kuwa jumla ya watahiniwa waliofaulu vizuri yaani daraja la I hadi la III wako 173, 422 sawa na asilimia 35.8 wakiwemo wasichana 75,056. Tazama matokeo yote hapa>>>

“Mwaka 2020 watahiniwa waliopata madaraja ya juu ya daraja la I, II na la III walikuwa 152,909 sawa na asilimia 35.1 hivyo ubora wa ufaulu wa matokeo haya kidato cha nne 2021 umeongezeka kwa asilimia 0.74,” amesema Dkt. Msonde.


Watahiniwa 10 bora Kidato cha Nne


1. Consolata Prosper Luguva - St. Francis Mbeya
2. Butoi Ernest Kangaza - St. Francis
3. Wllhemia Steven - St. Francis 
4. Cronel John - St Francis
5. Merry George Ngoso - St Francis
6. Holly Beda Lyimo - Bright Future Girls
7. Brandina - St. Francis 
8. Imamu Suleiman - Feza Boys
9. Mfalme Hamis Madili - Ilboru
10. Clara Straton - St. Francis 

Shule 10 bora Kidato cha Nne

1. Kemebos - Mkoa wa Kagera
2. St. Francis - Mbeya
3. Waja Boys - Geita
4. Bright Future Girls
5. Bethel Sabs Girls - Iringa
6. Maua Seminary - Kilimanjaro 
7. Feza Boys - Dsm
8. Precious Blood - Arusha
9. Feza Girls - Dsm 
10. Mzumbe Secondary - Morogoro. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news