Simba SC yabaini hujuma, yatoa onyo kali

NA GODFREY NNKO

MIEZI kadhaa ikiwa imepita baada ya uongozi wa Klabu ya Simba kuingia makubaliano ya kimkataba na Kampuni ya Vunja Bei wenye thamani ya shilingi bilioni 2 ya kutengeneza na kuuza jezi kwa kipindi cha miaka miwili, wametoa onyo kali kwa watu ambao wamekuwa wakijihusisha na uuzaji au usambazaji wa jezi zenye nembo yao ambazo hazijasambazwa na mzabuni. 
Hayo wameyabainisha leo Januari 7, 2022 kupitia taarifa kwa umma waliyoitoa huku ikitoa onyo kali kwa wenye tabia za kufanya hujuma ya namna hiyo kama inavyosomeka hapa chini;
Aprili 20, 2021 akitangaza rasmi mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez alisema ni mkataba wa kihistoria kwa Tanzania, kwani haijawai kutokea kuingiwa kwa mkataba wenye thamani kubwa kama hiyo Afrika Mashariki na Kati.

Gonzalez alisema kuwa, mkataba huo utakuwa umempa nafasi ya kuuza bidhaa zote zinazohusiana na Simba kama jezi, kofia, soksi na vifaa vingine vya klabu hiyo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Vunjabei Group Limited, Fred Fabian Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei aliishukuru klabu ya Simba kwa kuichagua kampuni hiyo kwa sababu kulikuwa na makampuni mengi, lakini waliamua kuipa nafasi kampuni yao kwa kuthamini ubora wa kazi zao.

Pia aliwaomba mashabiki wa Simba kuanza utaratibu wa kununua bidhaa rasmi za klabu ili kupata vifaa halisi na vyenye ubora mkubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news