"Tuliharibiwa kwa kusema mwananchi ataungiwa umeme kwa 27,000,gharama za umeme haziko hivyo,kuna maeneo tutafanya hivyo kuwabeba wananchi,kuna maeneo lazima gharama ya umeme irudi pale pale,Waziri umeogopa kusema,nakusaidia nenda katekeleze.
"Kuna maeneo lazima gharama ya umeme ibebe uhalisia unapompangia TANESCO aende akaunge umeme kwa elfu 27 kwa kila mtu yeye anatoa wapi hizo fedha? Hana pa kuzitoa lazima aunge umeme kwa gharama inayopaswa kwa kila pahala, Waziri nenda kasimamie hilo,"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo Januari 4,2022 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Chini ni gharama za kuunganisha umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO);