NA GODFREY NNKO
UONGOZI wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) limehairisha safari ya treni ya abiria ambayo ilitakiwa kuondoka jijini Dar es Salaam kwenda jijini Arusha leo.
Safari hiyo ilipaswa kuanza leo Januari 17, 2022 kuanzia saa 8:30 mchana ambapo kwa sasa imepangiwa kuondoka Januari 19,2022 muda huo huo.
"Shirika la Reli Tanzania (TRC) linautaarifu umma kuwa treni ya abiria iliyotakiwa kuondoka Dar es Salaam saa 8:30 mchana siku ya Jumatatu tarehe 17, 1, 2022 kuelekea Arusha, haitaondoka.
"Treni hiyo itaondoka siku ya Jumatano tarehe 19,1, 2022 saa 8:30 mchana. Shirika linaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza,"imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa kwa umma na TRC leo Januari 17, 2022.