NA GODFREY NNKO
TUME ya Madini nchini imetoa taarifa ya bei elekezi kwa baadhi ya madini yanayozalishwa nchini na kuuzwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2022.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na tume hiyo ikieleza kuwa, wana ina jukumu la kutoa bei elekezi za madini kulingana na hali ya masoko ya madini husika ndani na nje ya nchi, kwa ajili ya tathmini na uthaminishaji wa madini pamoja na ukokotoaji wa mrabaha.
"Bei hizi zimeanza kutumika kuanzia Jumamosi ya tarehe 1 Januari 2022. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafutayo
"Mrabaha unatozwa kwa bei zinazojumuisha gharama zote hadi kufikia sehemu ya mauzo. Bei elekezi za madini ya dhahabu zitaoneshwa katika vibao kwa maandishi makubwa katika masoko husika.Bei elekezi za madini pia zinaweza kutegemea ankara za malipo zilizowasilishwa Tume ya Madini,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo kama inavyoonesha bei hapa chini (kama unatumia simu kuza picha uweze kusoma kwa ufasha);
BEI ELEKEZI KWA MUJIBU WA TUME YA MADINI KWA BAADHI YA MADINI YANAYOZALISHWA NCHINI NA KUUZWA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI JANUARI HADI
MACHI 2022 (INDICATIVE PRICES OF MINERALS WITH REFERENCE TO PREVAILING LOCAL AND INTERNATIONAL MARKETS FOR SELECTED MINERALS RODUCED IN TANZANIA FOR THE PERIOD OF JANUARY TO MARCH 2022)