Vigogo Simba SC watozwa faini kwa kauli tata, Yanga SC nayo mlango wawagharimu

NA GODFREY NNKO

KAMATI ya Uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Desemba 30,2021 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanya maamuzi.
Maamuzi hayo ni pamoja na mechi Namba 64 kati ya Simba SC na Yanga SC katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara ya NBC (NBCPL) ambapo Yanga imetozwa shilingi milioni 1 kwa kosa la kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kutumia mlango usio rasmi katika mchezo huo uliochezwa Desemba 11,2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na bodi hiyo, adhabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17 (21,60) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo ikizingatiwa kuwa hii ni mara ya pili kwa klabu hiyo kutenda kosa la aina hiyo msimu huu.

Wakati huo huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ametozwa faini ya shilingi 500,000 kwa kosa la kuituhumu Bodi ya Ligi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa ilimzuia yeye na familia yake kuingia uwanjani kutazama mchezo huo. "Jambo ambalo halina ukweli".

"Barbara hakukubaliana na maelekezo halali ya maafisa wa mchezo huo kuhusu utaratibu wa kuingia eneo la watu maalum (VVIP) ndipo akaamua kuondoka, adhabu hii ni kwa kuzingatia kanuni ya 46 (10) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa viongozi.

Katika hatua nyingine,Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu ametozwa faini ya shilingi 500,000 kwa kosa la kutoa matamshi yenye utata kupitia vyombo vya habari kuwa kama Bodi ya Ligi na TFF zimepanga kuipa klabu ya Yanga ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC basi zifanye hivyi na kumaliza msimu mara moja.

"Adhabu hii ni kwa kuzingatia kanuni ya 46(10) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa viongozi,"imefafanua taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine Bodi imechukua hatua mbalimbali kwa timu na viongozi wao kulingana na makosa mbalimbali kama inavyoonekana hapa chini;




Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news