NA GODFREY NNKO
YUAN ya China inanunuliwa kwa shilingi 358.5 huku ikiuzwa kwa shilingi 361.98 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.75 na kuuzwa kwa shilingi 19.94.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 10, 2022 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa mujibu wa BoT, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 146.29 na kuuzwa kwa shilingi 147.7 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.197 na kuuzwa kwa shilingi 20.36.
Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205.
Dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2,286.39 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.25. Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3095.77 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3127.19.
Wakati huo huo, kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2583.16 na kuuzwa kwa shilingi 2609.914.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania