NA GODFREY NNKO
LEO Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 14, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 148.75 na kuuzwa kwa shilingi 150.16 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.2 na kuuzwa kwa shilingi 20.33.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.45 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.32.
Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3137.70 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3167.77.
Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2621.19 na kuuzwa kwa shilingi 2647.63.
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.47 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.01 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 20.0022 na kuuzwa kwa shilingi 20.20.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania