NA GODFREY NNKO
YUAN ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.942 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.47 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 20.115 na kuuzwa kwa shilingi 20.311.
Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.17 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 17, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 148.84 na kuuzwa kwa shilingi 150.28 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.17 na kuuzwa kwa shilingi 20.34.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.49 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.36.
Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2617.35 na kuuzwa kwa shilingi 2644.45.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania