NA GODFREY NNKO
EURO ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2594.0511 na kuuzwa kwa shilingi 2620.915.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 20, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3118.1203 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3149.5325.
Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 360.34 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.88 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.97 na kuuzwa kwa shilingi 20.17.
Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.655.
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 149.24 na kuuzwa kwa shilingi 150.694 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.17 na kuuzwa kwa shilingi 20.34.
Pia kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.
Dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.515 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.38.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania