NA GODFREY NNKO
LEO Januari 25,2022 kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 149.971 na kuuzwa kwa shilingi 151.409 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.15 na kuuzwa kwa shilingi 20.321.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2,286.58 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.45.
Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2584.07 na kuuzwa kwa shilingi 2610.8332.
Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 361.51 huku ikiuzwa kwa shilingi 365.061 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 20.095 na kuuzwa kwa shilingi 20.29.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania