NA GODFREY NNKO
LEO Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2286.67 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.44.
Wakati huo huo, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2545.75 na kuuzwa kwa shilingi 2572.135.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 31, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3058.65 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3090.395.
Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.67 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.81 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.781 na kuuzwa kwa shilingi 19.98.Aidha, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.66.
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 146.28 na kuuzwa kwa shilingi 147.71 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.15 na kuuzwa kwa shilingi 20.31.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania