Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 5, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 142.33 na kuuzwa kwa shilingi 143.7 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.22 na kuuzwa kwa shilingi 20.39.

Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT leo Januari 5,2022 kuhusu viwango elekezi vya kubadilisha fedha mbalimbali za kigeni, dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2,286.21 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.07.

Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3082.27 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3113.32.

Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2577.24 na kuuzwa kwa shilingi 2605.94.

Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 358.54 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.07 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.66 na kuuzwa kwa shilingi 19.85.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news