NA GODFREY NNKO
LEO Januari 6,2022 kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 142.33 na kuuzwa kwa shilingi 143.7 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.22 na kuuzwa kwa shilingi 20.39.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2,286.21 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.07.
Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3082.265 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3113.32.
Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2577.24 na kuuzwa kwa shilingi 2605.94.
Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.55 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.66 na kuuzwa kwa shilingi 19.85.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania