NA ANGEL MNDOLWA
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila, Prof. Lawrence Museru amewakabidhi vyeti wataalamu 45 wa dawa za usingizi na ganzi, ngazi ya cheti kutoka katika hospitali za wilaya na mikoa mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na wahitimu 45 waliopatiwa mafunzo ya dawa za usingizi na ganzi. Mafunzo hayo yametolewa na MNH.
Prof. Museru amewataka wahitimu hao , kuwa mabalozi wazuri huko waendako na kutekeleza yale waliyoyapata hapa kwa kueneza mazuri waliyojifunza.
“Serikali imefanya maboresho makubwa katika sekta ya afya kuanzia ngazi ya Taifa hadi zahanati hivyo ikaja na mpango wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi kwa ngazi ya cheti ili kupunguza uhaba wa wataalamu hao nchini,”amesema Prof. Museru.
Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza Prof. Museru.
Mkuu wa Idaraya Uzingizi na Ganzi wa Muhimbili, Dkt. Moses Mulungu akieleza machache kuhusu mafunzo hayo.
Wahitimu wa kifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi, amesema jukumu la MNH ni kutoa fursa kwa wataalamu kuja kujifunza na kuhakikisha inazalisha watu ambao watakuwa bora katika utendaji kazi.
Naye, Mkuu wa Idara ya Usingizi na Ganzi, Dkt. Moses Mlungu, amesema mafunzo hayo ambayo wataalamu wamejifunza kwa muda wa miezi 6 yamehusisha mafunzo kwa vitendo na nadharia ili kuwajengea uwezo.
Mwakilishi wa wahitimu hao, Bw. Mohamed Tillika akishukuru uongozi wa Muhimbili kwa kuandaa mafunzo hayo.
Baadhi ya wataalamu wa usingizi na ganzi wakiwa kwenye kikao hicho.
Bw. Peter Wawae akipokea cheti kutoka kwa Prof. Museru Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Sufiani Baruani na kulia kwake Dkt. Mulungu.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na Prof. Museru.
“Wizara ya Afya, TAMISEMI kushirikiana na MNH imeandaa progamu maalumu kwa ajili ya wataalamu hao, ambapo tangu kuanzishwa kwake imetoa mafunzo kwa wataalumu zaidi ya 300 kutoka hospitali mbalimbali nchini.”ameongezea Dkt. Mlungu
Wahitimu hao, wanatoka mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mtwara, Geita, Lindi, Pwani, Katavi, Chato, na Dar es Salaam.