Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, wakikagua eneo linalotarajiwa kujengwa Tawi jipya la BoT mkoani Kigoma, baada ya kufanya kikao kifupi kutathmini mwenendo wa sekta ya fedha ya mkoa huo. (Picha zote na BoT).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi baada ya kikao kifupi mkoani Kigoma.
Majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
Jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.
Majukumu mengine ya Benki Kuu ya Tanzania;
>Kutoa sarafu ya nchi ambayo ni Shilingi ya Tanzania
>Kusimamia na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha
>Kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini.
>Kusimamia akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni
>Benki ya Serikali
>Benki ya Mabenki; na
>Kutoa ushauri juu ya masuala ya uchumi na fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.