Waziri Prof.Ndalichako atoa rai kwa watumishi wa wizara yake

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka watumishi wa ofisi hiyo kushirikiana ili kuleta maendeleo katika Taifa na sekta hiyo ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo walipokuwa wakipokelewa rasmi Januari 10, 2022 katika Ofisi hiyo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo Januari 10, 2022 alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya viongozi kuteuliwa kuongoza Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni wakiwemo na Naibu Waziri Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Katibu Mkuu, Prof. Jamal Katundu.

“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kutupa nafasi mimi pamoja na Naibu Waziri na Katibu Mkuu ya kuwepo katika Ofisi hii ya Waziri Mkuu,” alieleza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili rami katika ofisi yake hii leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipowasili katika ofisi hiyo. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi. (Picha na OWM).

“Niwaombe watumishi kuimarisha ushirikiano ili maeneo haya yote manne yaani Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu yatekelezwe ipasavyo,” alisema Waziri. Prof. Ndalichako.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news