Yanga SC yapokonywa Kombe la Mapinduzi saa chache baada ya Manara kujigamba

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

PENGINE muda huu, mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam, Yanga SC wanaendelea kupanga kila kilicho chao kurejea Tanzania Bara.
Ni baada ya mabingwa wa kihistoria kwenye Kombe la Mapinduzi, Azam FC leo Januari 10, 2022 kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi mbele ya Yanga kwa ushindi wa penalti.  

Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote mbili kutoshana nguvu, hivyo mshindi kutafutwa kwa kupitia mikwaju ya penalti. 

Matokeo hayo mabaya kwa vinara hao ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara yanakuja ikiwa awali Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara alijigamba kuwa, kombe hilo wanalo na wanatarajia kuondoka nalo tena;

Ilikuwa ni moja ya mchezo wenye ushindani mkubwa ambapo Azam FC wao waliweza kupachika penalti tisa kimiani huku Yanga SC ikifunga penalti nane. 

Penalti tano tano za mwanzo zilikamilika kwa kila timu kufunga jambo lililopelekea kuweza kuanza kupigiana penalti mojamoja. 

Aidha, ngoma ilikuwa nzito kwa kipa Erick Johola kuweza kuokoa penalti sawa na Kigonya Mathias wa Azam FC, lakini ni Yassin Mustapha aliweza kukosa penalti na kuifanya Azam kushinda penalti ya mwisho kupitia kwa Mudhathir Yahya.

Mchezo mwingine ni ule wa pili ambao utazikutanisha Simba SC wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam dhidi ya Namungo FC ambao ni wenyeji wa Mkoa wa Lindi kuanzia saa 2:15 usiku. Mshindi katika mtanange huo atajumuika na Azam FC katika fainali hapo Januari 13, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news