NA MWANDISHI DIRAMAKINI
KLABU ya Yanga imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na wenyeji timu ya KMKM katika michuano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea jijini Zanzibar.
Mtanage huo uliopigwa leo Januari 7, 2022 katika dimba la Amaan, Yanga SC walienda mapumziko wakiwa na goli moja ambalo lilipatikana dakika ya 45.
Heritier Makambo kwa pasi ya Dikson Ambundo dakika ndiye aliyepeleka kilio kwa KMKM, hivyo hadi kipindi cha kwanza kinatamatika mambo kwao yakawa hayapo vema.
Kipindi cha pili upepo ulibadilika, KMKM ilibadili shangwe ya Yanga SC ambapo Abdlahaman Ali katika dakika ya 55 alibadilisha matokeo, hivyo ubao ukasoma moja kwa moja.
Dakika ya 81, Feisal Salum aliwanyanyua mashabiki wa Yanga SC kupitia bao safi ambalo lilifanya ubao kusoma mabao mawili kwa moja.
Zikiwa zimesalia dakika chake, Yanga wakiwa na ndoto za kutwaa alama tatu zote, KMKM ndani ya dakika ya 90 walivuruga mipango kwa kuachia bao la pili, hadi mwisho wa mtanange ubao ulisoma mabao 2-2. Kwa matokeo hayo, Yanga SC inasonga mbele kwa ajili ya nusu fainali.
Jana, Kenneth Muguna dakika ya 67 aliipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Kundi A Kombe hilo la Mapinduzi usiku katika dimba la Amaan jijini Zanzibar.
Huku mechi iliyotangulia ya Kundi A pia, Meli 4 City iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Yosso Boys huku mabao yakifungwa na Hussein Mwinyi dakika ya 18, Said Omar dakika ya 45 na Ali Mmanga dakika ya 81.