Ziara ya Rais Dkt.Mwinyi huko UAE yaonyesha matokeo ya haraka uwekezaji

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dokta Hussein Ali Mwinyi ameendelea na ziara yake katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.tHussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwekekezaji wa Kampuni ya Eagle Hills Regionals Properties ya (UAE) wakati wa utiaji wa Saini wa Miradi miwili mikubwa ya Uwekezaji Zanzibar, baina ya Kampuni hiyo na SMZ, hafla iliyofanyika Dubai katika Umoja wa Nchi wa Falme za Kiarabu.(Picha na Ikulu).

Baada ya kuwasili Abu Dhabi jana usiku kwa ziara ya siku tatu katika nchi za Falme za Kiarabu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Hussein Ali Mwinyi leo ameshuhudia utiaji saini wa miradi mikubwa ya uwekezaji baina ya Serikali ya Zanzibar na Kampuni ya Eagle Hills Regional Properties ya Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE. 

Kwa upande wa Zanzibar, utiaji saini huo ulifanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar-ZIPA na kwa upande wa Kampuni ya Eagle alikuwa Mheshimiwa Mohammed Ali Rashid Alabar. 

Mwekezaji huyo alimueleza Dokta Mwinyi kuridhishwa kwake na mazingira ya uwekezaji Zanzibar tofauti na alivyotembelea mataifa mengine duniani ambako nako amewekeza miradi mikubwa. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Mtawala wa Dubai Sheikh.Mohammed Rashid Al-Makhtoum,baada ya kumalizika kwa hafla ya utowaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la “Zayed Sustainability Prize Awards” na ufunguzi wa Wiki ya Uendelezaji wa Masuala ya Kibinadamu. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Maonesho wa Dubai,akiwa katika ziara ya kiserikali katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE. 

Alimshukuru pia Rais Dokta Hussein Mwinyi kwa kumuunga mkono na kuahidi atafanya kila linalowezekana kuhakikisha uwekezaji anaotarajia kuufanya unafanikiwa. 

Miradi inayotarajiwa kujengwa na mwekezaji huyo ni Hoteli ya nyota tano eneo la Kizingo ambapo pia mwekezaji huyo anatarajiwa kujenga nyumba Zanzibar kwa ajili ya maeneo ya makaazi. 

Vilevile chini ya mradi huo eneo jingine litakalonufaika na uwekezaji huo ni Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja ambako kutajengwa hoteli yenye hadi ya nyota tano na vilevile nyumba za kuishi zenye hadhi ya juu kwa ajili ya soko la watalii na watu wenye uwezo. 

Ziara hii ya Rais ilianza kuonesha dalili nzuri mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi ambapo baada tu ya kutoka ndani ya ndege mvua ya wastani lianza kunyesha. 

Mapema asubuhi Rais Dokta Hussein Mwinyi alihudhuria sherehe za kuwatunuku vyeti washindi wa mpango endelevu wa Abu Dhabi unaojikita kuendeleza masuala ya afya, chakula, nishati, maji na maendeleo ya elimu duniani sherehe iliyofanyika Dubai. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Dr.Sultan Jabir, wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la “Zayed Sustainability Prize Awards”lililofanyika katika ukumbi wa Maonesho Dubai, wa ufunguzi wa Wiki ya Uendelezaji wa Masuala ya Kibinaadamu. “Abu Dhabi Sustainability Week” (kulia kwa Rais ) Rais wa Korea Mhe.Moon Jae-in na Mtawala wa Dubai Sheikh.Mohammed Rashid Al-Makhtoum. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Dr.Sultan Jabir, wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la “Zayed Sustainability Prize Awards”lililofanyika katika ukumbi wa Maonesho Dubai, wa ufunguzi wa Wiki ya Uendelezaji wa Masuala ya Kibinaadamu. “Abu Dhabi Sustainability Week” .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Dr.Sultan Jabir,wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la “Zayed Sustainability Prize Awards” lililofanyika katika ukumbi wa Maonesho Dubai,wa ufunguzi wa Wiki ya Uendelezaji wa Masuala ya Kibinaadamu.“Abu Dhabi Sustainability Week”. 

Rais Dokta Mwinyi katika shughuli nyingine aliyoifanya leo ni kutembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya kimataifa ya Dubai yanayojulikana expo 2020. Rais anaendelea na ziara yake katika nchi za Falme za Kiarabu ziara inayotarajiwa kumalizika Jumatano tarehe 19 Januari, 2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza na kupata maelezo kutoka wa Afisa wa Banda la Maonesho la Tanzania wakati wa maonesho ya Expo Dubai 2020,yanayofanyika katika viwanja vya maonesho Nchini Dubai,baada ya ufunguzi wa Wiki ya Uendelezaji wa Masuala ya Kibinadamu na utowaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la “Zayed Sustainability Prize Awards” na(kulia kwa Rais) Balozi wa Tanzania Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) wakati wa ziara yake ya kiserikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news