40 wanaohusishwa na mauaji ya watu sita wadakwa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

JESHI la Polisi nchini limekamata silaha 11 pamoja na kuwashikilia watu 40 ikiwa ni muendelezo wa kufuatilia waliohusika na mauaji ya watu sita. Ni katika mapigano ya wakulima na wafugaji yaliotokea Kilindi mkoani Tanga, Januari 30, 2022.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Mihayo Msikela ameyasema hayo Februari 3, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi wilayani Kilindi.

Amesema kuwa,baada ya agizo la Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro mafanikio hayo yamepatikana kwa haraka.

"Kati ya watuhumiwa hao 40, watuhumiwa 27 wameachiwa huru, lakini 13 tunaendelea kuwashikilia na miongoni mwao wapo walioshiriki mauaji moja kwa moja, wamo waliotoa usafiri na kuitisha vikao,"amesema Kamanda Mihayo. 

Pia ametoa rai kwa wananchi wote nchini kusalimisha silaha wanazomiliki kihali na kuzitumia katika uhalifu na zile ambazo wanamiliki isivyo halali, vinginevyo baada ya siku saba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news