40 wapatiwa mafunzo kukabiliana na majanga mkoani Manyara

NA MOHAMED HAMAD

KUTOKANA na mabadiliko ya tabianchi yalisababisha vifo vya mifugo zaidi ya elfu 25,000 wilayani Kiteto mkoani Manyara Chama cha Msalama Mwekundu Tanzania, TRCS mkoani wameanza kukabiliana na maafa kwa kuelimisha volunteers 40 wa kukabiliana na majanga hayo.

Mafunzo hayo yametolewa na Tanzania Red Cross Society mjini Babati, ambapo imeelezwa kuwa yanahusu huduma ya kwanza, kukabiliana na majanga pamoja elimu ya lishe na kumtambua na.kumsaidia mtu mwenye tatizo la utapiamlo.
"Mafunzo haya yatapunguza maafa yanayoendelea kujitokeza kwa washiriki kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwani madhara zaidi yametajwa kuendelea kujitokeza ndani ya jamii yakiwemo maafa,"amesema.

Akieleza umuhimu wa mafunzo hayo Janeth Silyimbo mwezeshaji kutoka TRCS alisema, wanakusudia kuondoa tatizo la maafa kwa jamii kwa kutoa elimu na msaada.
Alisema wananchi wengi hawajui maana ya majanga na namna ya kukabiliana nayo akisema watakaopata uelewa watapunguza maafa hayo kwa jamii.

Mratibu wa TRCS Mkoa wa Manyara Claudia Hauli aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuyathamini kwa yamelenga kuondoa tatizo ambalo linaleta madhara vikowemo vifo vya watu na mifugo.
"Wilaya ya Kiteto na Simanjiro imepata madhara makubwa sana kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamesababisha zaidi ya mifugo 25, 000 kufa"alisema Claudia.

Mratibu wa maafa Mkoa wa Manyara Samwel Dahaye amethibitisha maafa hayo akisema Serikali kwa kushirikiana na mashirika ya umma kikiwemo chama cha msalaba mwekundu wamekuwa wakipunguza adha kwa wananchi kwa kutoa elimu na misaada.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Esuputi Lamnyaki alishukuru kupatiwa mafunzo hayo akisema alipoteza ngombe 5 kutokana na ukame akidai angekuwa na uelewa kukabiliana na majanga hayo angeokoa mifugo yake.

Daniel Mollel (mshiriki wa mafunzo) alisema mafunzo hayo yatapunguza madhara kwa jamii haswa maeneo ya vijijini ambapo watakutana na waelimishaji tofauti na watu wa mjini ambao wana fursa nyingi kama vyombo vya habari kuwaelimisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news