NA MWANDISHI DIRAMAKINI
KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametangaza Wasemaji wa Kisekta 24 (Baraza Kivuli la Mawaziri) watakao kuwa na jukumu la kuisimamia Serikali kwa kuhakikisha changamoto zizonazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Katika Baraza hilo limezingatia usawa wa kijinsia ambapo wanawake wapo 12 sawa na wanaume huku nafasi ya Waziri Mkuu akiteuliwa, Dorothy Semu atakayekuwa mtendaji mkuu wa shughuli zote zitakazokuwa zifanywa na Baraza hilo litakalokuwa linafanya shughuli zake nje ya Bunge kuona Serikali inatekeleza wajibu wake.
Akitangaza majina mengine ya watakaounda baraza hilo kivuli Februari 6, 2022 jijini Dar es Salaam, Zitto amewateua wafuatao na wizara zao kwenye mabano; Abdul Nondo (Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Msemaji Mkuu wa Baraza Kivuli), Emanuel Mvula (Wizara ya Fedha na Uchumi), Fatma Fereji (Mambo ya Nje), Masoud Salim (Wizara ya Ulinzi) na Mbarala Maharagande (Wizara ya Mambo ya Ndani).
Wengine walioteuliwa ni; Riziki Mngwali (Wizara ya Elimu), Wizara ya Afya (Dk Nasra Omar), Mwanaisha Mndeme (Wizara ya Uwekezaji, Mashirika ya umma na Hifadhi ya Jamii), Pavu Abdallah (Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Muungano) na Kulthum Mchuchuli (Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini).
Katika uteuzi huo, Zitto pia maewatangaza; Isihaka Mchinjita (Wizara ya Nishati), Edgar Mkosamali (Wizara ya Madini), Halima Nabalang'anya (Wizara ya Viwanda na Maendeleo ya Biashara), Esther Thomas (Wizara ya Maji na Mazingira),
Wakili Victor Kweka (Waziri wa Katiba na Sheria), Mtutura Mtutura (Wizara ya Kilimo Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Bonifasia Mapunda (Ardhi na Maendeleo ya Makazi), Injinia Mohammed Mtambo (Miundombinu ya Ujenzi Barabara na Reli) na Ally Saleh Alberto (Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi).
Wengine wanaounda Baraza hilo ni pamoja na; Juliana Makan'gwali (Wizara ya Maliasili na Utalii), Wakazi Wasira (Utamaduni, Sanaa, Ubunifu na Michezo), Mwalimu Macheyeki (Vijana, Kazi na Ajira) na Janeth Rithe (Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto).