Benki Kuu ya Tanzania yatoa onyo kali kwa waliotoa taarifa feki ya ajira, wananchi watakiwa kuwapuuza

DAR ES SALAAM-Kuna barua pepe feki inayosambaa mitandaoni kuhusu kuwepo kwa mchakato wa ajira Benki Kuu wa kuchukua wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali za Fedha. Taarifa hizi hazina ukweli wowote, hivyo zipuuzwe.

Barua pepe hiyo feki ya tarehe 5 Februari, 2022 yenye kichwa cha habari “OMBI LA KUKUAJIRI BOT” ambayo inaonesha kutumwa kupitia barua pepe ya Benki Kuu ya info@bot.go.tz imemtaka aliyeandikiwa kuwasilisha maombi yake ya ajira kupitia barua pepe ya esamson048@gmail.com.

Aidha, taarifa hiyo feki inaonesha kuwepo kwa mawasiliano kati ya mtu aitwaye Irene Millinga (millingairene42@gmail.com) na mtu aitwaye Dr. Tefilo Richard (tefilor1@gmail.com ) tarehe 8 na 9 Februari, 2022 kupitia barua pepe yenye kichwa cha habari “MCHAKATO WA AJIRA BOT”.
Taarifa hizi zote ni za uongo. Bila shaka zimeandaliwa na watu wenye nia ovu ili kuwatapeli watu kwa imani kuwa watapata ajira Benki Kuu. Hakuna mchakato wowote wa ajira unaoendelea Benki Kuu kwa kuchukua wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali za Fedha.

Hivyo, taarifa hizo zipuuzwe. Aidha, tunawaonya watu wanaojihusisha na kutunga taarifa za uongo za namna hii kuacha mara moja kuepuka hatua za kisheria dhidi yao. 

Imetolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki botcommunications@bot.go.tz


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news