NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya GSM, Gharib Said Mohamed (GSM) ameamua kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti na Ujumbe wa Kamati ya Ushindi ya Timu ya Taifa Stars na kuwatakia Watanzania wote kila la kheri.
Haya yametangazwa kwenye mkutano na waandishi wa habari jioni hii ambapo pia kumetangazwa Kampuni ya GSM kujitoa kwenye sehemu ya Wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania.
Wachambuzi wa soka nchini Tanzania, wameidokeza DIRAMAKINI BLOG kuwa, hii inaweza kuwa ishara mbaya kwa Klabu ya Yanga ambayo GSM imekuwa ikiiunga mkono kwa nguvu zote, hali ambayo imeiwezesha kustawi zaidi kwa sasa.
"Sisi kama GSM pamoja na kuwa na plan nyingi za kusaidia timu in terms of technical bench na wachezaji ambazo tayari tumezifanya kwa kiasi kikubwa... tumemleta pia mtaalamu mwingine kutoka South Afrika ambaye ataongezeka katika technical bench kuungana na Luc, Riedoh. Hii yote ni kuifanya Yanga SC kuwa na nguvu.
"Tunaendelea na tutaendelea kufanya vitu vingine ambavyo vipo nje ya mkataba , lengo ni kuendelea kuisaidia timu yetu ya Yanga SC. Tukizungumzia kambi ambayo timu inakaa na uwanja wa kufanyia mazoezi ni 100% GSM inasimamia,"aliwahi kuyasema haya hivi karibuni Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Mwekezaji wa Kampuni ya GSM na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga.
Tags
Michezo