Kaimu Meneja Ufundi, Mhandisi Mathew Ndossi akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kuhusu maboresho yaliyofanyika ya barabara ya kuruka na kutua ndege na maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi akitoa maelekezo kwa uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea uwanja huo mkoani Kilimanjaro.
Meneja TEHAMA wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Magati Munyambo akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kifaa kinachotumika kutolea risiti za maegesho ya magari katika uwanja huo wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea uwanja huo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Kitengo cha Mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), David Katondo akifafanua kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi namna mizigo inavyotunzwa na kusafirishwa.
Mwongoza Ndege Mkuu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Norbeta Seneor akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kifaa kilichokuwa kinatumika kuandika taarifa za ndege, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro.