'Lowassa' awapa tano viongozi wanawake Tanzania

NA ANNETH KAGENDA

WADAU mbalimbali wameendelea kutoa pongezi zao kwa viongozi wanawake wanaoongoza mihimili na taasisi mbalimbali nchini Tanzania akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na kusema kuwa viongozi hao wana uwezo mkubwa wa kuongoza nchi.
Katibu Mkuu wa Vijana kutoka Tanzania Peace Foundation (TPF) Taifa, Charles Sabinian maarufu kama Lowassa (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Vijana kutoka Tanzania Peace Foundation (TPF) Taifa, Charles Sabinian maarufu kama Lowassa, alisema kuwa wao kama vijana wamekuwa wakijivunia uongozi wa akina mama ambao awali haukupewa kipaumbele kikubwa.

"Kwa wakati huu ambao viongozi wengi tena wa ngazi za juu ni akina mama sisi kama vijana tumekuwa tukipata faraja kubwa kutokana na kwamba kama unavyojua akina mama wanahuruma," amesema Katibu Lowassa.

Lowassa ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema hivi karibuni Rais aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa na kusema kuwa yeye kama kiongozi wa vijana kwa kushirikiana na vijana wenzake nchini wanampongeza Rais na kumuombea Mungu ampe umri mrefu.
"Mimi kama Kiongozi wa Vijana TPF Taifa, nakutana na vijana kwenye vikao mbalimbali sina shaka na uongozi wa Rais wala Spika wa Bunge Dkt. Ackson na ninaamini viongozi hawa ni wachapakazi na ndio maana wameaminiwa na kupewa uongozi wa nchi," amesema Katibu huyo na kuongeza;

"Kwa upande wangu ambaye ni kiongozi wa Taasisi pia nampongeza sana Rais wa nchi kwa maendeleo makubwa anayoyafanya kwenye nchi ikiwemo kuendeleza miradi tena mikubwa iliyoachwa awali na watangulizi wake akiwemo Rais wa Awamu ya Tano na ni kiongozi anayesimamia kauli zake na kuzisimamia,"amesema.

Amesema kuwa, anampongeza pia Spika wa Bunge Dkt. Ackson kwa ushindi wa kishindo na kwamba anawapongeza pia wale wote waliomchagua na kusema kuwa yeye kama kijana anayekutana na watu mbalimbali wakiwemo vijana, rika la kati pamoja na wazee aliiona nyota ya Spika iking'ara mapema.

Hata hivyo, hivi karibuni Lowassa alikuwa ni mmoja wa Majaji kwenye mashindano ya vipaji vya wasanii wanaojulikana kama Quality Group High Level ambapo aliwaasa vijana kuchapa kazi ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono viongozi wote wa nchi hasa wanawake.

Mmoja wa wadau ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waigizaji Tanzania, Chiki Mchoma, alisema " Dunia ya leo vyombo viwili vya mihimili mikubwa Tanzania ina wanawake na Rais tangu awali amekuwa akishika nafasi kubwa na hilo ni jambo la kujivunia kama nchi,"amesema.

"Lakini kwa Spika picha ipo wazi kwamba ni mchapa kazi na ni wakati mwafaka kwa vijana hasa wanawake kuanza kujipanga kwenye misingi ya awali ya kupata uongozi tena mkubwa na siyo kubweteka," amesema Mwenyekiti Chiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news