Maafisa Biashara watakiwa kubadilika kifikra na kiutendaji katika kutekeleza majukumu yao

NA MWANDISHI MAALUM-BRELA

MKURUGENZI wa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Andrew Mkapa amewataka Maafisa Biashara kubadilika kifikra na kiutendaji na kuendeleza dhana ya kusaidia zaidi kuliko kufanya ubabe katika kutekeleza majukumu yao ya utoaji wa leseni za biashara.
Bw. Mkapa ametoa wito huo wakati akifunga mafunzo juu ya Sheria za Leseni za Biashara kwa Maafisa Biashara wa mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara na Simiyu. yaliyoendeshwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kwa muda wa siku tano mkoani Mwanza.

“Katika mapendekezo mengi mmetoa ushauri na maoni ambapo ukiangalia kwa asilimia kubwa yapo ambayo ya kisheria, yanahitaji mchakato wa kisheria, yapo ya kisera yanayohitaji uboreshaji wa Sera lakini pia yapo yakiutendaji yanahitaji mabadiliko ya utendaji katika ofisi zetu, lakini yapo mengine ya kifikra tu ambayo yanahitaji kubadilisha fikra na mitazamo,"amesema Bw. Mkapa na kuongeza kuwa;

Kwa yale ambayo hayahitaji kusubiri michakato mingine zaidi, kama mlivyokumbushwa katika mafunzo haya mkajitahidi kwenda kubadilisha ama utendaji, ama fikra zenu na mkaendeleze dhana ya kusaidia zaidi badala ya kuonesha ubabe na mkajiandae kisaikolojia kwa ajili ya mabadiliko ya mifuno, Mkapa

Akitoa ufafanuzi wa sheria Bw. Mkapa ameeleza kuwa; Kwamujibu wa Sheria ya Leseni ya mwaka 1972 imekuwa ikifanyiwa mapitio mara kwa mara, lakini kwa asilimia kubwa mapitio yaliyokuwa yanafanyika chini ya sheria za fedha ya kila mwaka yanagusa masuala ya makusanyo ya mapato kwa asilimia kubwa, lakini mabadiliko hayakutokea huko tu bali yalitokea maeneo mengi kwenye maeneo ya kijamii na kiutendaji hivyo kuna haja kubwa ya kufanyiwa mapitio na marekebisho ya sheria hii.

Aidha aliongeza kuwa kwa muda mrefu sheria hii unaweza sema ilikuwa haitumiki (domant) ama ilikuwa ikitumika kifungu kimoja na kutolea mfano wa mwaka 2004 Ada za Leseni ziliondolewa ambapo mtu alikuwa akikata Leseni mara moja tu na alikuwa haihuishi kwa maana ya kurenew na ilikaa hivyo hadi mwaka 2014, ndio maana sheria hii inaonekana ina mambo mengi ya kizamani na haipewi kipaumbele cha kufanyiwa maboresho kama zilivyo sheria nyingine. 

Bw. Mkapa ameainisha kuwa moja ya sababu ambayo huenda imechangia kutofanyiwa marekebisho sheria ya Leseni ni wazo lililokuja la uanzishwaji wa sheria ya Bara (Business Activities Registration Act), ambayo kwa bahati mbaya haikuwahi kufanya kazi, lakini sheria hii katika vifungu vyake vya mwanzo ilionekana kuwa ilikuja kuchukua nafasi ya sheria hii ya Leseni za Biashara (Business Licence) hivyo kama ingepitishwa ingechukua nafasi na hii ndio sababu imefanya watu kutokuwa na msukumo wa kufanyia marekebisho kwa sheria iliyopo na kiuhalisia sheria hii inahitaji kufanyiwa marekebisho.

Hata hivyo Bw. Mkapa amebainisha kuwa kuna mchakato ambao umeanza kwa ajili ya kuifanyia marekebisho ili kuifanya iendane na wakati lakini pia kutoa toleo lililojumuisha marekebisho yote yaliyofanyika katika sheria hii (revise edition). 

Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku tano, yaliandaliwa na kutolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa biashara juu ya Sheria ya Leseni za Biashara yaliyoanza tarehe 7 Februari na kuhitimishwa tarehe 11 Februari , 2022 Jijini Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news