Maelekezo yatolewa kuwanufaisha wakulima wa tumbaku

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBUNGE wa Jimbo la Ushetu Wilayani Kahama Mhe. Emmanuel Cherehani ameshiriki mkutano mkuu wa nne wa Chama Kikuu cha Ushirika Milambo kilichopo mkoani Tabora akimuwakilisha Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe.
Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye manunuzi ni muhimu wote wanaohusika na mnyororo wa zao la tumbaku kuhakikisha bei inakuwa nzuri, kuteua madaraja kwa usahihi wa sokoni na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima ili mkulima aweze kurejesha mikopo na kuinuka kiuchumi.

Cherahani ametoa rai hiyo wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mkoani Tabora na kuhudhuriwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, wanunuzi wa tumbaku, taasisi za fedha pamoja na wawakilishi wa vyama vikuu vinavyolima tumbaku.

Mbunge Cherehani amewataka viongozi kuhakikisha wanasimamia malipo ya wakulima ili waweze kulipwa kwa wakati jambo litakalowafanya waweze kufanya maandalizi ya mashamba kwa ajili ya msimu unaofuata kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Mhe. Cherehani amempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua changamoto za wakulima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news