NA HAPPINESS SHAYO-WMU
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi kuacha kuomba kumegewa maeneo ya Hifadhi ili kuepukana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu.
Amesema hayo leo katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipompa nafasi ya kujibu kuhusu changamoto ya wanyama wakali na waharibifu mkoani humo.
Amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo, vikosi kazi vitatumwa katika maeneo yenye changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.
Aidha,ameahidi kutekeleza maelekezo ya Rais ya kuhakikisha Wizara inaweka Kambi ya kudumu kwenye maeneo yenye changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.