NA KADAMA MALUNDE
MIPANGO wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imekutana na wafanyabiashara za bajaji na pikipiki pamoja na wajasiriamali wanaofanya shughuli zao katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi pamoja na fursa mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali.
Mtaalamu wa Sheria MKURABITA, Harvey Kombe akizungumza na waendesha bodaboda na bajaji katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga wafanyabiashara za bajaji na pikipiki kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi Februari 9,2022. (Picha zote na Malunde 1 Blog).
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa waendesha bodaboda, bajaji na wafanyabiashara wa Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga, Februari 9,2022, Mtaalamu wa Sheria MKURABITA, Harvey Kombe amesema biashara ya bajaji,pikipiki na ujasiriamali ni biashara kama zingine hivyo wanapaswa kufuata taratibu,kanuni na sheria zilizowekwa na serikali.
Kombe amesema mafunzo hayo ni mwendelezo zoezi la utoaji elimu yatakayotolewa kuanzia Februari 9 hadi Februari 16,2022 kwa wafanyabiashara 2000 katika Manispaa ya Shinyanga kati yao 1000 ni wafanyabiashara wa bodaboda na bajaji na 1000 ni wafanyabiashara wengine wa kawaida ambapo Taasisi mbalimbali zitakuwa zinatoa elimu ya fursa zilizopo katika taasisi hizo.
Waendesha bodaboda na bajaji wakiwa katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga wakifuatilia mafunzo.
Afisa Oparesheni Trafiki Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Pallangyo akiwataka waendesha bodaboda na bajaji kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni za udereva na usafirishaji,kutobeba abiria zaidi ya mmoja na kuepuka mwendo kasi.
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga (DTO), Dezidery Kaigwa akiwataka waendesha bodaboda na bajaji kutambua alama za barabarani vikiwemo vivuko ili kuepuka ajali za barabarani akieleza kuwa wamekuwa hawasimami kwenye vivuko (Zebra).
Mmoja wa waendesha bodaboda wilaya ya Shinyanga akiuliza swali.
Maafisa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na MKURABITA wakiwa katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga.
Maafisa kutoka NSSF Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Nguzo Nane, Hassan Baruti akiwakaribisha maafisa kutoka MKURABITA na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuwaelezea wafanyabiashara katika soko hilo namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi.
Mtaalamu wa Sheria MKURABITA, Harvey Kombe akiwaelezea wafanyabiashara wa Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi.
Wafanyabiashara wakiwa katika soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Maafisa mbalimbali wakiwa katika soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Mjumbe wa Dawati la Uwekezaji Manispaa ya Shinyanga, Bestina Gunje akiwahamasisha wajasiriamali kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Afisa kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Shinyanga Sajenti Hellen Kiseru akitoa elimu ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto pamoja na kuhamasisha wananchi kutoa taarifa za matukio ya moto kwa kupiga simu namba 114 bure.
Miongoni mwa Taasisi zilizotoa elimu kuhusu Fursa walizonazo leo ni Benki ya CRDB,NMB, EXIM, TCCIA,SIDO,Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kombe ameeleza kuwa ili kutoa fursa zaidi kwa wafanyabiashara, MKURABITA kwa kushirikiana na Manispaa ya Shinyanga wameanzisha Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendeshaji na Uendelezaji Biashara na Uwekezaji Manispaa ya Shinyanga.
“Hapa Shinyanga tunaanzisha Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendeshaji na Uendelezaji Biashara na Uwekezaji Manispaa ya Shinyanga ambacho kitakuwa katika jengo la CCM wilaya ya Shinyanga ambapo ukatarabati unaendelea. Kupitia kituo hiki wafanyabiashara watapata mafunzo ya biashara,mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara na fursa za uwekezaji”,amesema Kombe.
Akizungumza katika mafunzo kwa waendesha bajaji na pikipiki, Afisa Oparesheni Trafiki Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Pallangyo amewataka waendesha bodaboda na bajaji kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni za udereva na usafirishaji,kutobeba abiria zaidi ya mmoja na kuepuka mwendo kasi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga (DTO), Dezidery Kaigwa amewataka waendesha bodaboda na bajaji kutambua alama za barabarani vikiwemo vivuko ili kuepuka ajali za barabarani akieleza kuwa wamekuwa hawasimami kwenye vivuko (Zebra).
Naye Afisa Mfawidhi Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA) Mkoa wa Shinyanga, Bahati Musiba amesihi waendesha bodaboda na bajaji kukata na kulipia ada ya leseni ya usafirishaji abiria ili kuachana na tabia ya kufanya shughuli ya usafirishaji kwa kificho huku akisisitiza kuwa ni marufuku kwa pikipiki ya magurudumu mawili kubeba abiria zaidi ya mmoja na magurudumu matatu abiria wanne.
Akizungumza katika Soko la Nguzo Nane,Afisa Maendeleo ya Jamii na Mjumbe wa Dawati la Uwekezaji Manispaa ya Shinyanga, Bestina Gunje amewashauri wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kujiinua kiuchumi kwani mikopo hiyo haina riba kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Mtaalamu wa Sheria MKURABITA, Harvey Kombe akizungumza na waendesha bodaboda na bajaji katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga wafanyabiashara za bajaji na pikipiki kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi.
Mtaalamu wa Sheria MKURABITA, Harvey Kombe akizungumza na waendesha bodaboda na bajaji katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga wafanyabiashara za bajaji na pikipiki kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi.
Afisa Mfawidhi Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA) Mkoa wa Shinyanga, Bahati Musiba akiwataka waendesha bodaboda na bajaji kukata na kulipia ada ya leseni ya usafirishaji abiria ili kuachana na tabia ya kufanya shughuli ya usafirishaji kwa kificho.
Tags
Habari