NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mao wilayani Kalambo mkoani Rukwa, Devota Kyando amesema kuwa, tukio hilo lilitokea Februari 13, 2022 majira ya saa 10 alfajiri ulipoanza ugomvi baina ya wanandoa hao.
Kyando amesema kuwa, kwa muda mrefu kulikuwa na mgogoro wa kifamilia baina yao hali iliyokuwa ilisababisha wafikishane kwenye Serikali ya kijiji kwa ajili ya usuluhishi na kuendelea kuishi pamoja.
Richard Mwanakulya ambaye ni baba mzazi wa mtuhumiwa wa mauaji hayo amesema kuwa, kwa muda mrefu mtoto wake alikuwa na ugomvi na mke wake, lakini walikuwa wakisuluhisha na mambo yanaonekana kutulia na kuendelea na maisha kama kawaida.
Amesema kuwa, mgogoro ulianza baada ya watoto wao kuolewa bila kulipiwa mahari, kitendo ambacho mtuhumiwa alikuwa akidai kinamuuma na mke wake ndiyo aliyosababisha kwa kuwa aliwalea vibaya watoto wake wa kike.
Mazwile amesema, mara kwa mara mtuhumiwa kila anaporejea nyumbani kwake kutoka kilabuni, huanza kumtukana mke wake akidai kuwa malezi yake mabaya kwa watoto ndiyo yamewatia aibu na kusababisha watoto wao kuchukuliwa kiholela na wanaume bila kulipiwa mahali.
Ndipo siku ya Februari 13,2022 majira ya saa 10 alfajiri alianza kumpiga mke wake, kipigo kilichomsababishia majeruhi makubwa kichwani na kumsababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale alikiri kutokea tukio hilo la mauaji na kusema kuwa polisi inamshikilia mtuhumiwa wa mauaji hayo.
Amesema kuwa, mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Pia aliwataka wanandoa na watu waliopo katika mahusiano ya kimapenzi kutatua changamoto walizo nazo mapema na kuwashirikisha viongozi wa dini, wazee wa ukoo ili kuepusha vitendo vya kujichukulia sheria mikononi na kusababisha mauaji.