WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umetoa pongezi maalum kwa Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetoa pongezi maalum kwa Bi.Zuhura Yunus Abdallah kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu).