Rais Samia aishirikisha Dunia fursa mbalimbali za uwekezaji kutoka Tanzania

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini huku akiwahakikishia mchakato mzima umerahisishwa na unatekelezwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Ustahimilivu na Uhusiano ambaye pia ni Kamishna wa Maonesho ya Dubai Expo 2020 Sheikh Nahayan Mabarak Al Nahayan wakati akielekea katika Banda la Maonesho la Tanzania lililopo Dubai leo tarehe 26 Februari, 2022.

Mheshimiwa Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 26, 2022 wakati akihutubia kwenye Siku ya Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Expo 2020 Dubai yaliyofanyika Falme za Kiarabu (UAE) huku akiwakaribisha kutembelea banda la Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, pamoja na wananchi kutoka Mataifa mbalimbali Duniani katika Siku ya Kitaifa ya Tanzania katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 yanayofanyika Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE leo tarehe 26 Februari, 2022.

“Nichukue nafasi hii kuwakaribisha wafanyabiashara na wageni wote nchini kwetu, niwahakikishie kwamba kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na utalii,” amesema Rais Samia.

Pia amesema, wawekezaji ambao watataka kuwekeza nchini, usajili wa kampuni, taratibu za uhamiaji, kupata ardhi, leseni za biashara na kodi, yote yanapatikana katika kituo cha pamoja cha huduma kinachoitwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Ustahimilivu na Uhusiano ambaye pia ni Kamishna wa Maonesho ya Dubai Expo 2020 Sheikh Nahayan Mabarak Al Nahayan mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania pamoja na la Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika maonesho hayo ya Dubai Expo 2020 leo tarehe 26 Februari, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda mbalimbali ya Umoja wa Falme za Kiarabu UAE katika maonesho hayo ya Dubai Expo 2020 leo tarehe 26 Februari, 2022.

“Tanzania imefungua milango yake kwa mtu yoyote atakayetaka kutembea, kuwekeza au kufanya biashara. Inatoa hamasa kubwa ya uwekezaji na mtakutana na roho nzuri za Watanzania; na kwa sababu hiyo tunatabasamu wakati wote,” amesema Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha kumbukumbu mara baada ya mazungumzo na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE na Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum leo tarehe 26 Februari, 2022. (PICHA NA IKULU).

Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza kwamba, Serikali itaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) kuhakikisha ushirikiano wa kihistoria, kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa na kijamii unalindwa na kuendelezwa kwa manufaa ya pande zote mbili.

“Tanzania ni nchi yenye amani na ina mazingira bora ya kuvutia wawekezaji hivyo nawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini,”amesema Rais Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news