NA GODFREY NNKO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu.
Pia Mheshimiwa Rais Samia amesema kuwa,atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine kwani hiyo ndiyo kanuni ya uongozi bora.
Mheshimiwa Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 22, 2022 wakati akishiriki Jubilee ya Miaka 25 ya Utumishi wa Kiaskofu (1997-2022) ya Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge mjini Ngara Mkoa wa Kagera.
Rais Samia alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na Askofu Niwemugizi aliyoitoa akimuomba Mheshimiwa Rais kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote.
“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu, lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile usikubali. Ninakumbuka sana Hayati Benjamin Mkapa, najua huko mlikuwa mmezoea mtukufu rais, mtukufu rais alifika mahali akawa mkali kabisa mtukufu ni Mungu tu naomba hilo liwe neno kwako.
...basi nakuombea Mungu akusaidie kukuza upendo kati ya Watanzania unaotuongoza, ukuze haki nayo haki izae amani na utulivu na kukuza demokrasia katika nchi yetu.Ukuze upendo na mshikamo wa Watanzania ili hatimaye utumishi wako utukuke na kuacha alama itakayoonwa kwa vizazi vingi.
"Mungu akujalie hekima na uvumilivu wa kusikiliza hata yale yanayokera masikio yako, unajua sisi watoto wako tuko wakorofi, Mungu akujalie tu hekima na uvumulivu hasa pale unapokuwa ni ushauri wenye nia njema ya kulijenga Taifa letu liendelee kuheshimika ndani na nje,"amefafanua Baba Askofu Niwemugizi.
Kwa upande wake Mheshimiwa Rais Samia amesema kuwa, "Baba Askofu umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hiyo si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine, maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie, na sio nijitukuze kwenu.
"Nitajitahidi na Mungu anisaidie kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikio la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine, nakushukuru sana Baba Askofu kwa maneno hayo.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia amesema kuwa, "Kumekuwa na matukio mengi ya mauaji na watu kujiua kwa kipindi hiki yanaongezeka siku hadi siku, takwimu zinaonesha katika wilaya hii ya Ngara pekee mwaka 2020 kulikuwa na matukio 22 ya mauaji, matukio matatu ya watu kujiua, mwaka 2021 kulikuwa na matukio 21 ya mauaji na matukio mawili ya watu kujiua.

"Kuna sababu nyingi zinazofanya kuongezeka kwa matukio ya vifo na mauaji, na huwa tunaunda Tume ndani ya Jeshi la Polisi kuchunguza sababu za mauaji, ripoti zinapokuja wanasema, wivu wa mapenzi, imani za kishirikina, msongo wa mawazo, visasi, ugomvi wa kifamilia, ugumu wa maisha na mambo kama hayo.
"Ukiangalia sababu zote hizi za mauaji zinakuonesha kwamba watu hawako karibu na Mungu, kwa sababu anayeua, anayejiua kwa sababu yoyote ile wa dini yoyote ile hakuna dini iliyotoa ruhusa kufanya hayo, na tunafunzwa kuamini kwamba kifo kinapotokea ni kazi ya Mungu sasa sina hakika wanaojiua au kuua wenzao kama ni kazi ya Mungu sina hakika.
"Baba Askofu umezungumzia mmomonyoko wa maadili na kusahau mila na desturi ambako kumeondosha utu wetu, tuna kazi kubwa viongozi wa dini kurudisha tena nyoyo za watu kuthamini utu, kurudisha tena watu kumjua Mungu, kwa sababu kama unamjua Mungu huendi kumuua mwenzio kwa urithi, kisasi au kwamba umeambiwa amekuloga hukuvuna huendi kumuua mwenzio kama kweli unamjua Mungu, nitoe wito kwa viongozi wa dini, turudi kwenye mafundisho yetu tuisaidie jamii.
"Nizungumze pia na viongozi wa kimila na Machifu wenzangu, tuna kazi kubwa ya kufanya tena hapa, kuwaambia watu kwamba kinachotokea sicho tulichoamrishwa kwa dini wala mila na desturi zetu, hakuna mila zinazoamrisha watu wakauane,"amefafanua kwa kina Mheshimiwa Rais Samia.

Baba Askofu ameeleza nini?
Wakati huo huo, Askofu Niwemugizi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan atoe agizo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itoe msamaha wa zaidi ya shilingi milioni 326 inazodai katika hospitali teule za Wilaya ya Ngara na Biharamulo mkoani Kagera.
Amesema, Hospitali ya Ngara inadaiwa na TRA zaidi ya shilingi milioni 213 huku Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo ikidaiwa na mamlaka hiyo zaidi ya sh.milioni 113.
"Hospitali hizi mbili teule zinahudumia watu maskini wengine wanashindwa kumudu gharama za matibabu, kwa hakika zikifungwa hospitali hizi wananchi wataumia, tunaomba madeni tuliyonayo ya TRA tusamehewe. Pia Mheshimiwa Raisa, tunaomba tusaidie kupata vibali vya ajira ili kuboresha huduma, tutoe huduma bora kwa wananchi,"amefafanua Baba Askofu Niwemugizi.
Pia Askofu Niwemugizi amemuomba Rais Samia kusaidia eneo la Kanisa la Jimbo la Rulenge-Ngara lililotwaliwa na Halmashauri ya Wilaya Ngara lirejeshwe chini ya umiliki wa kanisa hilo.
"Eneo la ardhi lilipojengwa kanisa kuu la jimbo, sehemu yake ilichukuliwa na kujengwa kambi ya wakimbizi kwa maafikiano kwamba wakiondoka eneo litarudi kwa kanisa, lakini walipoondoka kanisa lilipotaka kulirejesha halmashauri ikalichukua. Pia eneo la Kanisa Kuu, upande wa pili lilipoanza kujengwa barabara nalo tulinyang'anywa isivyo haki, naomba turudishiwe eneo hilo,"amebainisha Askofu huyo.
Tags
Habari