NA MWANDISHI DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameitaka Mahakama kuzingatia sheria ili kutenda haki kwa watu wote bila kujali hali ya mtu kijamii na kiuchumi.
Amesema, anatambua mageuzi yanayoendelea katika mahakama yameongeza uwazi na uwajibikaji kwa watendaji wa mhimili huo lakini bado yapo malalamiko kwa wananchi ya kucheleweshewa haki na wakati mwingine kunyimwa kabisa.
Pia Rais Samia ameitaka mahakama kutoa haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi ambayo wananchi wengi hawafahamu na wanategemea mawakili ndio wawaongoze.
“Utu wako unakutumaje uchukue fedha uminye haki ya mtu? Au umpe aliyetumia umahiri na vifungu kumyima haki mwenye haki,”amehoji.