NA MWANDISHI DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini kuelekea Ufaransa na baadae Ubelgiji kwa ajili ya ziara ya kikazi katika nchi hizo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 9,2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Amesema kuwa, Rais Samia akiwa nchini Ufaransa anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.
Pia Rais Samia atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za miradi ya maendeleo, ushirikiano katika masuala ya uchumi wa buluu, usalama wa bahari, sekta ya usafiri na maendeleo endelevu.
Aidha,pamoja na masuala mengine, Rais Samia anatarajiwa kuzungumza na Watanzania waishio nchini Ufaransa.
Tags
Habari