RC Kunenge azindua mfumo wa anuani za makazi, atoa onyo

NA ROTARY HAULE

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,amezindua mfumo wa anuwani za makazi kwa wananchi wake huku akiwapiga marufuku wataalamu wanaosimamia zoezi hilo kuacha kuwashurutisha wananchi kutoa fedha kwa ajili ya kuchangia gharama za utekelezaji wake.
Kunenge amezindua mpango huo Februari 10, 2022 katika viwanja vya Mabatini vilivyopo Ikwiriri wilayani Rufiji ikiwa ni siku mbili baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaelekeza Wakuu wa Mikoa nchini kusimamia mpango huo kikamilifu.

Akizungumza kabla ya kuzindua mpango huo, Kunenge amesema kuwa mfumo wa anuani za makazi ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa na hivyo lazima kila kiongozi ajitoe katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.

Amesema,suala la anuani za makazi linasimamiwa na Rais Samia moja kwa moja kwa kuwa lipo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo lazima wasaidizi wake wawe mstari wa mbele katika kulisimamia.

Amesema, utekelezaji wa mpango huo unagharimiwa na Serikali kwa sh.bilioni 28 na kwamba hakuna sababu ya kuwalazimisha wananchi wachangie kwani kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu.

Amesema,maagizo ya Rais ya Februari 8, mwaka huu amewataka wakuu wote wa mikoa kusimamia jambo hilo ili kusudi ifikapo Mei mwishoni liwe limekamilik,a lakini kwa Mkoa wa Pwani lazima likamilike Aprili 30, 2022.

"Sisi Mkoa wa Pwani tumepanga zoezi hili likamilike April 30, mwaka huu na imani yangu tutafanikiwa kwakuwa utaratibu uliotumika kujenga madarasa ndio utakaotumika kutekeleza zoezi la anuani za makazi,"amesema Kunenge.

Kunenge amesema kuwa, hakuna kipande chochote nchini kilichokosa viongozi wa CCM kwa hiyo hakuna sababu ya kushindwa na endapo kama kuna sehemu itashindikana basi viongozi wake hawatoshi.

Amewataka Wakurugenzi,Wakuu wa Wilaya pamoja na ngazi zote za uongozi kujipanga kikamilifu ikiwa pamoja na kuwashirikisha wananchi pindi zoezi hilo linapoanza hili kusudi pasiwepo na malalamiko.

Amesema,katika utekelezaji huo hasitokee mtu kuwalazimisha wananchi kuweka majina ila kinachotakiwa majina yapendekezwe na wananchi wenyewe ila wataalamu wanaweza kutoa ushauri pale inapobidi.
"Tukikamilisha zoezi hili vizuri litakuwa limempa heshima nzuri Rais Samia,kwahiyo wataalamu lazima wafanyekazi usiku na mchana na muhimu zaidi ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwakuwa jambo hili ni jema,"ameongeza Kunenge.

Hatah ivyo, Kunenge amesema zoezi hilo pia litasaidia kufanyika kwa Sensa hapo Agosti 22 mwaka huu na kwamba wananchi lazima washiriki kikamilifu huku akiwakumbusha kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO-19 ikiwemo kujitokeza kuchanja.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowelle, amemshukuru Mkuu wa huyo wa Mkoa kwa kuiteua Wilaya yake kuwa sehemu ya uzinduzi wa mfumo wa Auani ya Makazi.

Gowelle amesema Wilaya ya Rufiji tayari imeandaa mpango kazi wake ambao utaanza Februari 22 na kumalizika Aprili 22 ambapo watafanya mikutano na wananchi,kuweka namba za nyumba ,kuweka Mitaa pamoja kuhamasisha viongozi wote kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo.

Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Mwanasha Tumbo,amesema Mkoa wa Pwani unakwenda kutekeleza zoezi hilo wakiwa na kauli mbiu "Pwani na Postikodi,Naweka Anuani yangu ya Makazi nipate maendeleo".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news