Serikali yaagiza kufutwa leseni 500 za utafiti wa madini Iramba

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Madini, Dkt.Lemomo Kiruswa ameagiza kufutwa kwa leseni za utafiti wa madini zaidi ya 500 ambazo hazifanyiwi kazi wilayani Iramba mkoani Singida.Naibu Waziri wa Madini, Dkt.Lemomo Kiruswa (wa pili kutoka kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mjiolojia, Agnetha Kato (kushoto) wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Madini katika kongamano la wadau kujadili fursa na changamoto kwenye sekta ya madini lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda mkoani Singida juzi. Wa tatu kulia ni mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Mwenda.

Pia wito huo umetolewa kwa wamiliki wa leseni za madini pamoja na wenye leseni za utafiti wa madini ambao hawazifanyii kazi kwa nchi nzima ambao wametakiwa wajiongeze na kuanza mara moja kuzifanyia kazi kabla ya wizara hiyo haija chukua hatua za kuwafutia.

Dkt.Kiruswa alitoa agizo hilo jana wakati akifungua kongamano la wadau kujadili fursa na changamoto kwenye sekta ya madini lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda mkoani Singida.

Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Iramba akimpigia saluti Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Lumomo Kiruswa (katikati) mara baada ya kuwasili viwanja vya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwenye kongamano la wadau kujadili fursa na changamoto kwenye sekta ya madini lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda (wa kwanza kushoto) lililofanyika wilayani humo jana.
Naibu Waziri wa Madini Dk.Lemomo Kiruswa (wa pili kutoka kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mjiolojia Mbeleye David wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Madini katika kongamano la wadau kujadili fursa na changamoto kwenye sekta ya madini lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda mkoani Singida jana. Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Mwenda.
Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida,Chone Malembo, akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya madini mkoani hapa.

Alisema Wilaya ya Iramba ina jumla ya leseni 694 za uchimbaji mdogo lakini ni leseni 102 pekee ndizo zinazofanya kazi, leseni za uchimbaji wa kati zikiwa tano (MLs) ambapo nne ni za Kampuni ya Sunshine ya Kichina ya Mining Ltd ambayo imeanza kuzalisha tangu Desemba 2021 na hadi kufikia Januari 2022 imeweza kuzalisha kilo 23.4 za dhahabu yenye ubora wa juu.

Alisema kutokana na uzalishaji huo Serikali kuu ilipata jumla ya Sh.200 Milioni ikiwa ni mrabaha na ada ya ukaguzi na Halmashauri ya Iramba ilipata Sh.10 Milioni ambapo pia ina leseni za utafiti wa dhahabu na almas (13) na leseni za uchenjuaji wa dhahabu 26.

Alisema kufuatia leseni hizo kutofanya kazi Waziri Kiruswa aliiagiza Tume ya Madini kuanza zoezi la kuzifuatilia ili utaratibu wa kuzifuta uweze kufanyika na kuwapatia watu wengine wenye nia ya kufanya kazi na Serikali iweze kupata mapato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Javan Diamonds Project (JDP) inayojishughulisha na Utafiti wa Almasi, Javan Bidogo ambaye pia ni mmiliki wa mradi wa utafutaji wa Almasi katika Kijiji cha Mbelekese kilichopo wilaya humo akitoa taarifa ya mradi huo kwenye kongamano hilo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kongamanohilo.
Kongamano likiendelea.
Maswali yakiulizwa kwenye kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo wa Wilaya ya Iramba, Ramadhani Masoud akiuliza swali kwenye kongamano hilo.
Mchimbaji wa madini Yusuph Kityapi akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Mchimbaji wa madini Wilfred Shalua akiuliza swali kwenye kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Wachimbaji Wilaya ya Ikungi, Seleman Dude akichangia jambo.M
Mjiolojia Charles Moe, kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambaye alimwakilisha Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi hiyo akichangia jambo kwenye kongamano hilo..
Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana Wa Ccm Mkoa Wa Singida Dr. Denis Nyiraha Akitoa maono Ya Vijana Katika Kongamano Hilo
Vijana wa Sisi Tanzania Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja katika kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Wadau wakiwa kwenye kongamano hilo.

Aidha Dk. Kiruswa alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa wilaya hiyo Suleiman Mwenda kwa kuwa wa kwanza mkoani hapa kuandaa kongamano la namna hiyo na akaomba na mkoa nao ufanye hivyo jambo litakalosaidia kuwaunganisha wadau wote wa sekta ya madini mkoani hapa.

"Niseme ukweli tu kuwa wewe Mwenda ni DC pekee ndani ya Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kufanya kongamano kubwa la namna hii lenye lengo la kuinua uchumi wa wananchi wa Iramba na Taifa kwa ujumla" alisema Kiruswa.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akitoa taarifa ya uchimbaji wa madini katika wilaya hiyo alisema akiwa msimamizi mkuu wa masuala ya uchumi na maendeleo hasa katika sekta ya madini alisema mchango wa mapato yatokayo na madini katika wilaya hiyo ulikuwa mdogo sana.
Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Mmojawa kada wa ChamaCha Mapinduzi (CCM) kupitia UVCCM Mkoa wa Dodoma, AsiaNdula (kushoto) akiwandani ya kongamano hilo
Kongamano hilo likifanyiwa dua na Sheikh Omari Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza kwenye kongamano hilo.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakiwa kwenye kongamano hilo.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kongamano hilo.
Taswira ya kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.

Alisema Wilaya ya Iramba ambayo tangu ukoloni ilijulikana kuwa na utajiri mkubwa wa madini ambapo mgodi wa kwanza ulianzishwa miaka 1909 Sekenke ambapo hadi leo uchimbaji wa madini unaendelea katika kipindi cha mwaka 2019 hadi 2022 jumla ya gramu 1,037,000 (sawa na tani 1.1) zenye thamani ya Sh.109.5 zimezalishwa ambapo kodi ya Serikali kuu ni Sh.7.69 Bilioni ikiwa ni mrabaha na ada za ukaguzi.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imeweza kukusanya jumla ya Sh.328.4 Milioni ikiwa ni ushuru wa huduma uliotokana na uzalishaji huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Javan Diamonds Project (JDP) inayojishughulisha na Utafiti wa Almasi, Javan Bidogo ambaye pia ni mmiliki wa mradi wa utafutaji wa Almasi katika Kijiji cha Mbelekese kilichopo wilaya humo akitoa taarifa ya mradi huo kwenye kongamano hilo alisema kampuni yao ambayo ni ya wazawa imejikita kufanya utafiti wa Almasi katika wilaya za Ikungi na Iramba tangu mwezi Machi mwaka juzi na kuwa wapo katika hatua nzuri ya utafiti.

“Tumefanya uvumbuzi katika baadhi ya miamba inayokuwa na Almasi jumla yake ipo 13 na kati ya hiyo tisa ni mikubwa ambayo tumekuwa tukiifatilia sana,”. alisema Bidogo.

Bidogo alisema kwa hivi sasa wamechukua sampuri ya udongo na kuanza kuziosha kwenye mtambo wao uliopo kwenye mradi ili waweze kuziona Almasi zote ambazo zipo kwenye udongo huo ambao wameuchukua kutoka maeneo mbalimbali wilayani Ikungi na Iramba.

Bidogo akizungumza kiutaalamu na umahiri wa juu huku akionesha uzoefu wa masuala yote ya uchimbaji wa almasi alisema kazi wanayoifanya kuyabaini madini hayo si nyepesi kwa kuwa hayaonekani kirahisi ambapo hutumia gharama kubwa na changamoto wanayokabiliana nayo vifaa (mitambo) ambayo inagharama kubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news