NA EMMANUEL MBATILO
TUME ya Madini imekabidhiwa magari saba kati ya magari 40 yanayotarajiwa kutolewa na Serikali kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akikata utepe ishara ya kuzindua magari saba na kuyakabidhi Tume ya madini kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.Zoezi hilo limefanyika Februari 21,2022 kwenye ofisi za zamani za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kabla ya kuzindua magari hayo Februari 21, 2022 Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko mbali na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa magari hayo yatatumika kama kichocheo cha ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini.
Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kununua vifaa vingine kama vile mashine za kupima madini kwenye masoko ya madini na kusimamia kwa karibu shughuli za madini ili kuhakikisha Serikali inapata mapato yake stahiki.Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akzungumza mara baada ya kukabidhi magari saba Tume ya Madini kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.
Aidha, amewataka watendaji wa Tume ya Madini kuhakikisha magari yanatunzwa na kuendelea kuchapa kazi kwa ubunifu mkubwa ili kuhakikisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 650 kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 linafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Katika hatua nyingine akizungumzia mikakati iliyowekwa na Wizara ya Madini kwenye udhibiti wa utoroshaji wa madini, Dkt. Biteko amesema kuwa mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuongeza maafisa kwenye usimamizi wa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akizungumza mara baada ya kupokea magari saba kutoka Serikalini kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.
Magari saba ambayo yamekabidhiwa Tume ya Madini kama moja ya mikakati ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO).
Waziri Biteko amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuwa Serikali haitamwonea huruma mtu yeyote ayakayebainika anatorosha madini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula sambamba na kuishukuru Wizara ya Madini kwa ununuzi wa magari kwa ajili ya kutumiwa kwenye shughuli za madini amesema kuwa magari yatarahisisha kwa kiasi kikubwa utendaji kazi kwa kufika maeneo yasiyofikika kirahisi.