NA MWANDISHI MAALUM
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi),Mhandisi Godfrey Kasekenya amemtaka mkandarasi wa kampuni ya CHICO kukamilisha ujenzi wa barabara za maingilio ya Daraja la Kitengule linalounganisha wilaya za Karagwe na Misenyi mkoani Kagera ifikapo mwezi Mei, 2022.
Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Luptan inayosimamia ujenzi wa Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140,Mhandisi Lucas Nyaki, akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi),Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati akikagua maendeleo yaliyofikiwa katika daraja hilo, mkoani Kagera.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi),Mhandisi Godfrey Kasekenya, akimsikiliza Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Luptan inayosimamia ujenzi wa Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140,Mhandisi Lucas Nyaki, wakati alipofika kukagua ujenzi wa daraja hilo, mkoani Kagera.
“Mkandarasi,
Msimamizi wa mradi na Wakala wa Barabara (TANROADS), hakikisheni
ifikapo tarehe 26 mwezi Mei mwaka huu mnakabidhi hii barabara kwa
kiwango cha lami,”amesisitiza Naibu Waziri huyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi),Mhandisi Godfrey Kasekenya, akikagua ujenzi wa Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 18 unaotekelezwa na mkandarasi CHICO na Mhandisi Mshauri Luptan kwa fedha za ndani kiasi cha shilingi Bilioni 25.5, mkoani Kagera.
“Serikali
iliamua kulijenga hili daraja kwa makusudi kwa kuwa tuna uhitaji mkubwa
wa sukari lakini pia kutazalisha sukari ambayo itakuwa ya bei chini
kwasababu ya kupungua kwa gharama ya usafirishaji wake,”amefafanua
Kasekenya.
Kasekenya ameeleza mipango ya Serikali ya Awamu ya
Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa upande wa
miundombinu ya barabara za kimkakati katika mkoa huo ambapo Serikali
imekwisha tangaza zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa barabara ya
Omurushaka – Nkwenda – Kaisho – Murongo;sehemu ya Kyerwa - Omurushaka
(km 50), Omugakorongo – Kigarama – Murongo (km 50), Bugene – Burigi –
Chato - Kasulo/Benako (km 60) kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
Magari ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera yakipita juu ya Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140 ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 97.4. Daraja hilo linaunganisha Wilaya ya Misenyi na Karagwe mkoani Kagera.
Aidha,
usanifu wa barabara ya sehemu iliyobaki ya Kitengule-Bunazi KM 25 ili
kuziunganisha Wilaya za Misenyi na Karagwe unaendelea kwa ajili ya
kujengwa kwa kiwango cha lami.
Amesisitiza kuwa azma ya Serikali
ni kufungua mkoa huo na mikoa jirani na pia kuunganisha nchi yetu
Tanzania na nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda kwa barabara za
lami. Muonekano wa sehemu ya barabara unganishi zenye urefu wa KM 18 pamoja na Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140, mkoani Kagera.
Awali
akitoa taarifa ya mradi, Meneja wa TANROADS mkoa wa Kagera Eng. Yudas
Msangi, ameeleza kuwa mpaka sasa ujenzi wa barabara unganishi umefikia
asilimia 76 na ameahidi kumsimamia kwa karibu Mkandarasi ili barabara
hiyo ikamilike kwa muda uliopangwa.
Naye, Meneja wa Mashamba ya
Kiwanda cha Sukari cha Kagera upande wa Kitengule Bw. Libehat Emmanuel,
amesema uwepo wa daraja la Kitengule ni msaada mkubwa katika kiwanda
hicho kwa kuwa miwa mingi ilikwama kutokana na miundombinu wezeshi ya
barabara na daraja na sasa wamekwisharuhusiwa kupita juu ya daraja na
miwa yote imepelekwa kiwandani kwa ajili ya uzalishaji. Muonekano wa Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140 ambalo ujenzi wake. (Picha zote na WUU).
Ameongeza kuwa uwepo wa daraja hilo na barabara unganishi utasaidia uaandaji wa mashamba ya sukari kwa upande wa Kitengule na Misenyi hadi kufikia ekta 16,500 ambayo itasaidia kuongeza uzalishaji wa sukari nchini hadi kufikia tani laki tatu (300,000), na hivyo kupunguza changamoto ya upungufu wa sukari nchini.
Ujenzi wa Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140 na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 18 unatekelezwa na mkandarasi CHICO na Mhandisi Mshauri Luptan kwa fedha za ndani kiasi cha shilingi Bilioni 25.5.