Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amiri akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kuhusu maendeleo ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Arusha wakati alipotembelea na kukagua mradi wa huo mkoani Arusha. Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Arusha, Elipid Tesha akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, eneo la mradi wa ujenzi wa sehemu ya maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Arusha, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea uwanja huo mkoani Arusha. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Arusha. Mradi huo umegharimu takribani Shilingi bilioni 1.9 na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2022. Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Arusha, Elipid Tesha akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, ramani ya jengo la abiria ambalo litajengwa katika Uwanja wa Ndege wa Arusha wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea uwanja huo mkoani Arusha. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), HAmis Amiri. (Picha na WUU).