NA MOHAMED OMARY MAGUO
UTENZI wa elimu na hamasa ya utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa maji katika kipindi hiki cha mvua;
1
Mikoa mingi yanyesha
Na maji kutiririsha
Tuvune yasijeisha
Tutumie kiangaziUvunaji wa maji ya mvua unaweza kumsaidia mkulima kuboresha kilimo chake na kujiongezea kipato zikiwemo faida nyingi katika maisha ya kila siku ya binadamu. (Picha na Mtandao).
2
Mapaa yetu safisha
Na gata kuzitayarisha
Mvua inaponyesha
Maji safi kisimani
3
Mabwawa kutegesha
Ili maji kukingisha
Tusiyaache yake'sha
Makorongo kubakisha
4
Mkondo kutopindisha
Mito kuinawirisha
Kwa maji kuijazisha
Huo ndio uzalendo
5
Sijaribu kuchepusha
Mvua inaponyesha
Bali wewe yavunisha
Maji yanayopotea
6
Mmomonyoko komesha
Ardhi kuistawisha
Tuvune inaponyesha
Yatufae Kiangazi
MTUNZI
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mshairi wa Kisasa
Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
25/2/2022