Utabiri wa hali ya hewa saa 24 zijazo, TMA inatoa angalizo la mvua kubwa na upepo mkali

 
Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo Februari 21, 2022 unawasilishwa na mchambuzi Noel Mlay.


MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI


Jumanne 22-02-2022

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa angalizo la mvua kubwa na upepo mkali kwa maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Kwa mujibu wa TMA, huenda ukavuma upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Athari zinazoweza kujitokeza;

Baadhi ya makazi kujaa maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za usafirishaji na uvuvi, nyumba zenye mapaa yasiyoimara kuezuliwa, kuanguka kwa miti midogo na kukatika kwa matawi ya miti mikubwa. Tafadhali zingatia na ujiandae.

Jumatano 23-02-2022

TMA inatoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia),Tanga, Morogoro, Ruvuma, Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Athari zinazoweza kujitokeza

Baadhi ya makazi kujaa maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za usafirishaji na uvuvi, nyumba zenye mapaa yasiyoimara kuezuliwa, kuanguka kwa miti midogo na kukatika kwa matawi ya miti mikubwa. Tafadhali zingatia na ujiandae.


Alhamisi 24-02-2022

TMA inatoa la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Athari zinazoweza kujitokeza

Pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za usafirishaji na uvuvi, nyumba zenye mapaa yasiyoimara kuezuliwa, kuanguka kwa miti midogo na kukatika kwa matawi ya miti mikubwa. Tafadhali zingatia na ujiandae.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news