GODFREY NNKO
LEO Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.4 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.9 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 20.005.
Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2286.67 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.56.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 10, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Wakati huo huo, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2615.3 na kuuzwa kwa shilingi 2641.7.
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3105.8 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3137.31.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.245 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.624 na kuuzwa kwa shilingi 0.655.
Aidha, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 149.53 na kuuzwa kwa shilingi 150.99 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.14 na kuuzwa kwa shilingi 20.304.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania