NA GODFREY NNKO
RANDI ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 151.1 na kuuzwa kwa shilingi 152.5 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.15 na kuuzwa kwa shilingi 20.313.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 14, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.703 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.6.
Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3105.6 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3137.1 wakati Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2607.3 na kuuzwa kwa shilingi 2634.3.
Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.63 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.1 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.72 na kuuzwa kwa shilingi 19.91.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania