NA GODFREY NNKO
YUAN ya China inanunuliwa kwa shilingi 360.51 huku ikiuzwa kwa shilingi 364.1 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 19.97.
Aida, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 151.103 na kuuzwa kwa shilingi 152.463 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.14 na kuuzwa kwa shilingi 20.30.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 16, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.244 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.626 na kuuzwa kwa shilingi 0.656.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.743 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.61.
Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3096.93 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3128.136 wakati Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2593.4 na kuuzwa kwa shilingi 2619.8.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania