NA GODFREY NNKO
YUAN ya China inanunuliwa kwa shilingi 360.98 huku ikiuzwa kwa shilingi 364.50 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.91 na kuuzwa kwa shilingi 20.11.
Aidha, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 150.6 na kuuzwa kwa shilingi 152.1 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.13 na kuuzwa kwa shilingi 20.296.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 22, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.243 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.625 na kuuzwa kwa shilingi 0.67.
Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.802 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.7.
Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3111.9 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3143.9 wakati Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2593.55 na kuuzwa kwa shilingi 2618.704.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania